Lost Password? No account yet? Register
  • Narrow screen resolution
  • Wide screen resolution
  • Auto width resolution
  • Increase font size
  • Decrease font size
  • Default font size
  • default color
  • red color
  • green color
Member Area

kimmediagroup.com

Wednesday
Aug 27th
Home arrow Education arrow Education arrow Kukopa harusi, kuilpa matanga
Kukopa harusi, kuilpa matanga Print E-mail
User Rating: / 3
PoorBest 


         Methali hii ina funzo kwa kila mmoja aliye na nia ya kujifunza; kwani “Asiyejua maana, haambiwi maana”. Hapo awali niliwaza tu juu ya utamu wa lugha: hivi sasa nimejionea na kuonja uchungu wa methali hii. Kisa na maana ni kwamba nilijitosa ukumbini mwa deni macho  wazi! Kwa kifupi, methali yenyewe inatufunza ya kwamba ni rahisi sana kukopa kitu chochote, lakini kazi yenyewe ni kulipa. Fikiria jinsi ilivyo vigumu sana kwa mtu yeyote kupata mkopo wa aina yoyote. lnampasa mtu kuwa na watu kadhaa wa kumwekea nadhiri ya kwamba ataweza kutimiza maagizo ya mkopo huo. Kwa sababu ya masharti hayo makali, wengi hukataa kutia sahihi au kusimamia mkopo.
 
       Nchi hii tunamoishi, ni nchi ya majitu;mambo yake pia ni makubwa. Nimegundua ya kwamba ni rahisi mno kukopeshwa gari kuliko chakula.Unachohitaji tu ni nakala ya hundi ya mshahara wako, pamoja na kitambulisho.Mchuuzi wa magari hukusaidia kuchagua gari litakalokupendeza; pia kukuongoza kujaza vikaratasi kadha wa kadha na kutia sahihi yako.Baadhi ya maandishi huwa hayaeleweki. Unapokawia kusoma ukurasa fulani atakwambia hapana maana kusoma yote. Wanunuzi wengi nao huwa na hofu ya kuuliza, wasionekane kutojua!Muda huo wote moyo hudunda na mwili kusisimka.Ndipo mtu huanza kuhisi kwamba amejitia kitanzi.
 
    Mwishowe mchuuzi hukuarifu ya kwamba gari ni lako. Unajulishwa kiasi cha fedha cha kulipa kila mwezi kupitia akiba ya benki. Kutia sahihi ni kukubali masharti yote yanayohusiana na gari hilo; pia inamaanisha utaweza kulipia gari hilo kwa muda uliowekwa. Jambo la kusikitisha ni kwamba malipo ya gari hutolewa kwa akiba yako kila mwezi: uwe umepata mshahara au hujapata, hiyo mwenzangu ni shida yako!Ukipatwa na shida ya ghafla kama ugonjwa au kufutwa kazi, ndipo utajua kuwa gari si lako.Hofu ni kwamba benki iliyogharimia mkopo wa gari lako, huendelea kutoa pesa kwa akiba yako kila mwezi . Unapochelewa kulipa unatozwa faini kubwa sana.
 
Kwa muda huo wote unapolipia gari lako unajihisi kama mtu aliye gerezani.Mtu huonekana kiwiliwili tu, lakini akili yake imenaswa katika mkopo.Mtu hukosa hamu ya chakula na huwa hana raha ya kuishi. Anajua kuwa atakaposhindwa kulipa kwa wakati ufaao, gari huenda likatwaliwa na kampuni iliyoligharimia. Hata hivyo deni hubaki na kuzidi kuongezeka kwa kasi mno.
 
Gharama ya gari la mkopo huwa ni ya juu sana . Kwa mfano: gari aina ya Toyota Corolla iliyoundwa mwaka 1995, ni dola 10,000 (elfu kumi).Unapolininua gari hilo kwa pesa taslimu, linagharimu kiasi cha dola 2,500 (yaani elfu mbili mia tano)!. Haya ni makadirio tu, kutoa mfano na kukusaidia wewe msomaji kuona ya kwamba hii mikopo ni ujambazi mamboleo.
 
Nilinunua gari langu kwa njia ya mkopo kama huu. Ukweli ni kwamba nimejuta (na kutubu) mara kadha. Nimejiahidi tena sitarudi kufanya hivyo. Wahenga walisema: Mwenzako akinyolewa, chako tia maji. Kumbuka ya kwamba, wembe ulioninyoa mimi utakunyoa wewe, tusiposaidiana. Jitahidi kujua umakinike, kwa maana “Chuma hunoa chuma. 
 
 

 
Advertisement